Jumatano, 17 Desemba 2014

WANANCHI WA ILEMBO MPUI WAPATA MWAMKO KUHUSU VYAMA VYA UPINZANI.Hili limeonekana baada ya wananchi walio wengi kuwa wafuasi wa chama kikuu pinzani CHADEMA. pale walipokuwa wakitoa kero zao kuhusu chama tawala cha CCM ambapo miaka yote kilikuwa kikipitwa bila kupingwa. na katika uchaguzi wa mwaka huu wa ngazi za serikali za mitaa na vijiji inaonekana upinzani kuja juu tofauti na hali iliyokuwepo hapo awali. licha ya kwamba uchaguzi uliotakiwa kufanyika tarehe 14 DEC 2014. uliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali ambazo inadaiwa kuwa zilichangiwa na chama tawala.

WANANCHI WA KIJIJI CHA ILEMBO MPUI WATOKEO KERO ZAO KUHUSU MSITU. Baadhi wananchi wa kijiji cha ilembo wametoa malalamiko yao kuhusu msitu wa kijiji hicho ambao umekuwa ukivunwa kiholela huku ikidaiwa kuwa msitu huo ni mali ya halmasha. walipoulizwa na wananchi wavunaji hao wenye mashine mbalimbali katika msitu huo wamekuwa wakidai kwamba wamepewa vibali na halmashauri jambo ambalo limekuwa likiwapa hofu wananchi kuwa jambo hilo halina ukweli.